Tuesday, 29 October 2013

HAKUNA PUMBAVU MWEREVU WOTE N VIPOFU

Saturday, 6 July 2013

NI NGUMU KUWAELEWA



NI  NGUMU KUWAELEWA
intro
yeah!ha!a,a habari zinazotufikia kwa sasa,ameonekana tena!
na anachana,ccr,skia, skia tena,skia,skia hii aaah!
verse 1
Asubuhi linachamoka ,watu wanaondoka
Mishe mishe mishe hadi jasho ladondoka
Watu wanaokoka,wapo wanaofoka
Busy  busy busy hadi watu wanakonda.e
Wengine wametoka  mshukuru Maulana
Wengine ndo wanapunga upepo mwanana
Wengine wanaskumwa wakapime HIV
Wengine wanataftatafta tu t.v
Wengine wametoka kupunguza vitambi
Wengine ndo wanakwenda kuzivuta bangi
Wengine wanatafta passport za dubai
Wengine ndo wanakwenda kujitoa uhai
Wengine watu wazima  na  wanaitana bby
Wengine  wanabeba watoto kama begi
Wengine wamelala wamelewa ile chakari
Wengine wanauliziaulizia tu hospitali.


Chorus
Wengine wamesimama tu! Hawaketi
Wengine wamenuna mh! Hawacheki.
Wengine wanapenda ju!hawashuki,
Mwingine asipotaja duuh!,harithiki.


Verse 2
Watu wanatongoza hadi dada zao
Wengine wana talaka warudishwa kwao
Wengine wanathamini tu suti na tai
Wengine wanatumia kanisa kulaghai
Wengine ni maskini na bado wanaringa
Wengine ni tajiri na bado wanakopa
Wengine wanaogopa giza na hakukuchi
Wengine wanakatikakatika wakiwa uchi
Wengine wanapendanga refu na kipenga
Wengine wanapenda messi anavyochenga
Wengine hawajafikiria na tayari washasema
Wengine wanabisha eti pwani si Kenya
Wengine walishatoa kafara watoto wao
Wengine usiku kutwa kwenye mtandao
Wengine shoot kwanza lenga baadae
Badala ya madini wanaokota vigae


Chorus
Wengine wamesimama tu! Hawaketi
Wengine wamenuna mh! Hawacheki.
Wengine wanapenda ju!hawashuki,
Mwingine asipotaja duuh!,harithiki.



Verse 3
Wengine wanarukanga bila hata kuanguka
Wengine wanaanguka bila hata kuruka
Mwingine mwanaume na ametoboka skio
Wengine wamesoma bila mafanikio
Mwingine anazingua eti kazi ni kazi
Na bado polisi wanasaka majambazi
Mwingine kajitoa kamegwa na vibabu
Mwingine anakesha na mshhara kilabu
Wengine washacheka hadi kwenye msiba
Mwingine hana talanta anataka kuimba
Wengine nawachana wananiita miguna
Wengine snitch sijui ka wanavuna
Wengine wanaandamana hawajui kwanini
Wengine wanajiuzajiuza kwa vimini
Mwingine ni mzazi anajiita bikra
Wengine wamerithi na wanajiita hustler


Chorus
Wengine wamesimama tu! Hawaketi
Wengine wamenuna mh! Hawacheki.
Wengine wanapenda ju!hawashuki,
Mwingine asipotaja duuh!,harithiki.


Chorus
Wengine wamesimama tu! Hawaketi
Wengine wamenuna mh! Hawacheki.
Wengine wanapenda ju!hawashuki,
Mwingine asipotaja duuh!,harithiki.
yeah
outro
na umwambie hapo alipojipata wala asistuke,kote ni kwake,
zitakuja tu,asali na maziwa kwani si wote watoto wake,yeah