NITAOA NIKIKOSA CHAKUFANYA
Siko tayari,labda mida ikibadilika
Hili bahari, kuchafuka likome
kabisa
Nona hatari, huu mzigo mpenzi kujitwika
Mwisho wa safari, niachwe dume mi
nasikitika
Sijawa limbuka, nabishana na hizi
pepo
Wenzangu nipisheni,najiepusha na
hili tendo
Imenishinda, wekeza, kwenye hizi
biashara
Natabiri nitateleza, zikanizalie
hasara
Niacheni nipotoke,nyi jitoeni
kafara
Mtafeli niwaokote, enyi mnaniona
kafala
Siogopi majukumu, naogopa
kudhulumiwa
Nisitumwe kuzimu,kabla muda
niliopangiwa
Walioitana wapenzi, leo wanavuaana
mataji
Mi nona hilo siwezi,bara nibaki mtazamaji
Labda nitangoza,baadaye lakini sio
leo
Siku mtakaponipoza, mapenzi yana
jipya toleo.
No comments:
Post a Comment