Mna bahati mmekua na sio tena
watoto.
Kinyume na hivyo,
ningewafuata popote mlipo.
Mkononi na kiboko.
Kazi ya kuwafunza watu wazima
adabu.
Sitaki kusema imenishinda,
lakini imenipa taabu.
Mlinishauri Mbwa wangu akifa nijifanye hainihusu.
Nipigieni makofi sababu
mlilonituma nimelijaribu
Tatizo, ule mzoga umenichafulia
hewa pale pangu.
Kila siku nabana pua,
nimebadili umbile alilonipa Mungu.
Ukimwona anaenda kuogelea
amevalia Suti na tai,
Kama sio filamu anaigiza mwelekeze kua haifai.
Nitawaonya dhidi ya kula
kabla ya kujua pa kujisaidia.
Eti mnakula kwa macho tu,
ambayo hayana pazia?
Ndio hayana pazia lakini
si unachagua pa kuangalia?
Vingi vilivyo dukani (kama sio vyote) vinauzwa.
Na ukifanana na kahaba,
ndivyo utakavyoitwa.
Niliuliza maana ya neno
fashion na ilinjibu kamusi
Na si ajabu sikuona popote
mlipoambiwa mtembee uchi.
Na ule msemo wenu wa kujaribu
kuyamiza malalamishi,
Eti mind your busness sisi
tunaenda na wakati.
Kweli?
Hamwogopi mnafanya mwanamke
aonekane kama kifaa?
Kwa jinsi mnavyovaa?
Nitakuheshimu na kukuoa
ukinionyesha una akili,
Na sio ukinifumbulia mwili.
Vaa nguo mi sio
gynaecologist.
No comments:
Post a Comment