Kila Usiku wa jana upitao,
Unaniacha Mwenzenu na Mzigo kibao,
Mzigo wa hasira Moyoni Ninao,
Japo kila kuchao najilazimisha
kusahau,
Wakifungua vinywa vyao wadau,
Hawafanyi lolote zaidi ya
kunikumbusha,
Mimi ndo kitoweo chao,
Natumika kama mpira sababu,
Maishani sina dira,
Naamini aliyeniambukiza huu ujinga,
Ana uhusiano na mganga anayetaka
kuniganga,
Utaniambiaje wakimwaga mboga nimwage
ugali,
Wakati chakula chao ni maziwa na
asali?,
One, two, one, two, wanaandaa
vipaza,
Wakisubiri giza limeze mwangaza,
Ili
vifo vyetu waje kuvitangaza,
Ajabu naogelea kwenye damu bila
kujali
Alichinjwa nani,nikielezwa marehemu
Alinitanguliza nataka kubisha
haiwezekani,
Mwanasiasa hivi we umetumwa na
nani?,
Mbona uwe kama
balozi wa Shetani?,
Vijana imewashinda kutumia bongo
zao
Kwetu kuna giza kibao.,
Kwenu kuna stima?

No comments:
Post a Comment