Mi naskia skia tu!
Eti maisha kama
kioo ukiyachekea yanakuchekea,
Nimejaribu kucheka kwenye msiba
,sipendi picha ilivyotokea
Cameraman kutuamuru tutabasamu ili
atupige picha,
Haibadili chohote, itafahamika tu
kuna kitu tulificha.
Sishabikii saaana zile ndoto za
kitandani,
Maana nimeota mengi, mengi ambayo
hayawezekani.
Nataka kuishi kwenye uhalisi wa
dunia,
Ambapo ukijingonga kwenye ukuta
unaumia.
Tofauti kabisa na kitu
mnachoniambia.
Kila siku eti “the party don’t
stop”.
Wakati katika uhalisia tunastruggle kucope.
Maskini akijitita bill gate A.K.A tajiri,
Asitegemee msaada wowote wa kimali
Najua maneno yangu yanaonekana kama propaganda,
Lakini sioni ujanja wowote kuenda club
na hela ya msiba.
Sisemi tuomboleze kwenye harusi,
Nasema usimeze A.RV kama huna virusi.
Africa
kuna umaskini.
Kama
sio kwako basi kwa jirani.
Tumeendelea maana si dada zetu
wamejua vimini?
Na pia tunatongozana kwa simu za
mkononi?
Lakini wenzetu wanateseka ina maana
hawamwoni?
Kujiita tajiri haina maana endapo
utakosa kitu mfukoni
Sijali nitawapotezza marafiki
lolote na liwe.
Ishi kihalilisia ,kumbali una
shinda usaidiwe.
By chuma cha reli
No comments:
Post a Comment