Lile la ngombe kula nyasi halafu
anatoa maziwa nitakueleza linatokeaje,
Hili la binadamu kula ganda na
kutupa ndizi naomba tuliache!
Nawasikitikia waliishi vipi,
Hadi kufikia kutokwa na mvi,
Hawajashtukia maisha yameongezwa
chumvi,
Kwa kifupi, ni movie
,
Umeona kwa nini nimeliacha lile la
kula ganda na kutupa ndizi?
Ni kwa sababu ,kila kitu ni maigizo
siku hizi.
Utaelezeaje kinachompelekea mtu
timamu kujitia chizi?
Na mwanamke kuamini namuota na
nishamweleza sipati usingizi?
Mitaala feki ya elimu,
Binadamu kunywa sumu, eti kisa maisha magumu,
Mapenzi ya mtandao ambayo kwa
kawaida hayadumu,
Ni baadhi tu ya maigizo
yanayopatikana filamuni humu.
Aki ya nani huu movie lazima utauza.
Hata sioni haja ya kuuchuza
Wenyewe utajiuza,
Wenyewe utajiuza
,
Tatizo.
Sijui anayeturekondi alipo,
Tena kwa jinsi hali ilivyo,
Kitakuja kifo kabla ya malipo
Ndugu ,marafiki na jamaa, msinifanye
kushangaa,
Kwa kuniambiaa, kinachoendelea sio
kazi ya sanaa.
No comments:
Post a Comment