Wote kwa majina yenu,asanteni kwa kunifikiria,
Mlichoniambia nimekiskia na nitakizingatia.
Mmeniambia.
Nitembelee mtaalamu wa magonjwa ya akili,
Hilo
la kwanza halafu na la pili,
Nachokifanya nikikifanya nifanye japo kwa siri,
Unaona unafiki wenu ulivyokithiri?
Samahani nitawavunja moyo kwa kutotembelea mtaalamu,
Na nikimpitia sema ni ile tu kumpa salamu.
Nitawaambia tupo east Africa
na sio armsterdam,
Ili kuwathibitishia jinsi
gani navyojifahamu,
Yaani, nimekuja na ile akili yangu timamu.
Mida na misiba ya kulia ikitimia nitalia
Ila sio kwenye hii misiba ya kujitakia.
Hamna aliyepoteza msibani zaidi ya marehemu japo ametulia
Na wasioathirika sana
wanajilazimisha kulia
Hamjui wapo wanaovunja sheria kwa kuwa
Kitakachofuatia wapo tayari kukigharamia?
Niacheni basi mimi kicheko niangue,
Kutakavyokua na kuwe.
Maana daktari alisema kituflani kuhusu kucheka.
Eti kuwa maisha yangu yataongezeka
Sijali mtanichukia wote mnaoonywa bila kusikia
Na kiburi mnachojitia kwa mafanikio madogo tu mliyoyafikia
Kitakachofuatia,
Ni misiba ya kujitakia.
Nitoeni kwenye orodha ya watu msibani watakaolia
No comments:
Post a Comment