Kama
kwa kuivunja Sheria nitajisikia mtu huru,
Basi
pisheni njia jela naja kuishi na sio kuzuru,
Akili
imeniambia,
Nachokisema
ni muhimu zaidi ya hata navyokisema,
Nisiogope
kunena, kwa kuogopa binadamu watasema.
Sio
langu lengo kuonyesha umahiri wangu kwenye ushairi,
Nimetumwa
niandike chochote nachokipika kwenye akili,
Na
ndo maana,
T.V
zikipeperusha tuzo za mshairi bora ulimwenguni,
Mi
nitakua Sibanduki kwenye kutizama katuni.
Kama
kwenye ushairi nitakua sifuati masharti na kanuni,
Basi
nafaa nitokee kwenye vitabu vya kumbukumbu kwa ushairi mpya nilioumbuni
Ni
wajibu wangu kujenga kwangu kwa jinsi navyoamini,
Na
sio kubomoa kwa mwenzangu eti ndo tukeshe wote gizani.
Utanishtaki
vipi nitakapovaa suruali kichwani au tai kiunoni?
Yale
yale ya mwanafunzi kumchukia mwalimu anapofeli mtihani.
Ushairi
wangu sio majibu ya mtihani wala sishindani
Naandika
chochote kinachonitoka kichwani
No comments:
Post a Comment